SERA YA SIRI

Pigabet Online Sports Betting ("Pigabet") imejitolea kulinda taarifa zako binafsi kulingana na mahitaji ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi Na. 11 ya 2022. Sera hii ya   siri inakuwezesha kujua ni taarifa gani tunazokusanya unapotumia huduma zetu, kwa nini tunakusanya taarifa hizi na jinsi tunavyotumia taarifa zilizokusanywa.

Tafadhali kumbuka kuwa, Sera hii ya Siri itatumika kati yako na Pigabet. (‘Sisi’, au ’yetu’, kama inafaa). Sera hii ya Siri ni sehemu jumuishi ya Kanuni na Masharti ya Pigabet.

Mara kwa mara tunaweza kufanya mabadiliko ya Sera hii ya siri na kukufahamisha mabadiliko haya kwa kuchapisha masharti yaliyobadilishwa kwenye majukwaa yetu. Tunakushauri upitie Sera hii ya usiri mara kwa mara.

TAARIFA ZILIZOKUSANYWA

Tunazingatia maelezo ambayo yanaweza kutumiwa ili kumtambua mtu binafsi, ikijumuisha bila kufunga taarifa nyingine, jina la kwanza na la mwisho, tarehe ya kuzaliwa, Anwanini yoyote ya makazi, baruapepe, nambari ya simu, au taarifa nyingine muhimu kuwa Maelezo Binafsi (‘Maelezo Binafsi’). Unaweza ukatakiwa kutoa maelezo binafsi unapotumia tovuti yetu, kujisaji katika akaunti au kutumia huduma zetu. Maelezo binafsi tunayokusanya yanaweza kujumuisha maelezo yaliyotajwa hapo juu. Maelezo haya tunayahifadhi kwenye seva zetu. Unapojihusisha na huduma hizi, seva zetu huweka kumbukumbu ya shughuli ya kipekee kwako ambayo inakusanya habari fulani za kiutawala na taarifa za kiusalama ikiwa ni pamoja utambulisho halisi (source IP address), muda wa kutumia, tarehe ya kutumia, kurasa za wavuti zilizofunguliwa, matumizi ya lugha, ripoti za mwingiliano wa nakalatepe, na aina ya kisakuzi kilichotumiwa. Taarifa hii ni muhimu kwa utoaji na ubora wa huduma zetu. Hatukusanyi taarifa binafsi zinazokuhusu bila wewe kujua.

NJIA ZA KUKUSANYA NA KUCHAKATA DATA

Tunaweza kukusanya data fulani moja kwa moja kama ilivyojadiliwa hapo juu na kupokea Maelezo Binafsi kuhusu wewe unayetoa taarifa hizo kupitia huduma au mawasiliano mengine na maongezi kwenye tovuti. Tunaweza pia kupokea maelezo binafsi kutoka kwa wauzaji wa mtandaoni na watoa huduma, na kutoka kwa orodha ya wateja iliyopatikana kisheria kutoka kwa wauzaji wa upande wa tatu. Kwa kuongezea, tunaweza kuhusisha huduma za watoa huduma upande wa tatu kutoa msaada wa kiutaalamu kushughulikia miamala yako ya mtandaoni na kulinda akaunti yako. Tutaweza kuzitumia taarifa zozote unazotoa kwa wauzaji hao, watoa huduma, na huduma za biashara ya mtandao za upande wa tatu, na tutatumia taarifa binafsi kama ilivyoelezwa katika Sera hii ya Siri hapa chini. Taarifa hii itakuwa wazi tu kwa upande wa tatu nje ya kampuni kwa mujibu wa Sera hii ya Siri. Tunachukua hatua ili kuhakikisha kwamba mipango yetu na watoa huduma wa upande wa tatu na wafanyabiashara wa mtandaoni wanalinda siri zako.

Ili kuhakikisha usahihi wa taarifa, Pigabet itachukua hatua muhimu ili kuthibitisha kwamba data zilizokusanywa ni kamili, sahihi, na thabiti na maudhui ambayo yalikusanywa. Hatua hizo zinahitajika kabla ya kutumia data iliyokusanywa.

MATUMIZI YA TAARIFA

Tunatumia maelezo binafsi tunayokusanya kutoka kwako ili kutoa Huduma zetu, kutoa msaada kwa wateja, kuhakikisha usalama na kutambua ukaguzi wa ithibati, kuchakata shughuli zako zozote za mtandaoni, kusaidia ushiriki wako katika matangazo ya upande wa tatu, kukidhi mahitaji fulani ya biashara, na kwa madhumuni mengine yoyote yanayohusiana na uendeshaji wa Huduma. Kwa hivyo, tunaweza kutumia taarifa zako binafsi na za washirika wetu waliochaguliwa kwa uangalifu (ikiwa ni pamoja na washirika wingine ambao wana mipango ya kupeana  data na mhusika).

Maelezo yako binafsi tunaweza pia kuyatumia kukupatia (1) fursa ya matangazo na taarifa kuhusu bidhaa na huduma zetu; na (2) fursa ya matangazo na taarifa kuhusu bidhaa na huduma za washirika wetu, ili kupanua aina mbalimbali za bidhaa zinazotolewa na kuboresha huduma zetu kwa wateja. Mara kwa mara, tunaweza kuomba taarifa kutoka kwako kupitia tafiti au mashindano. Kushiriki katika tafiti hizi au mashindano ni kwa hiari kabisa na una uchaguzi kufichua au kutunza taarifa hizo. Taarifa zilizoombwa zinaweza kujumuisha taarifa za mawasiliano (kama vile jina, anwani ya mawasiliano, na namba  ya simu), na taarifa za demografia (kama vile msimbo anwani ya makazi, posta au umri). Kwa kukubali tuzo yoyote ya mashindano au ushindi kutoka kwetu, unakubaliana na matumizi ya jina lako kwa madhumuni ya kutangaza bila fidia ya ziada, isipokuwa kama sheria hairuhusu. Hata kama umechagua kutopokea taarifa za matangazo, tunaweza pia kutumia taarifa zako binafsi (ikiwa ni pamoja na baruapepe na namba ya simu) ili kukupa taarifa kuhusu bidhaa zetu, huduma, na matangazo, ikiwa ni pamoja na bidhaa nyingine za michezo ya kubahatisha ( pamoja na mchezo wa karata wa mtandaoni, kasino, kubashiri, backgammon)  bidhaa na huduma kutoka kwa upande wa tatu tuliowachagua kwa uangalifu.

Ingawa kunaweza kuwa na ulinzi wa ziada ambao unahitajika kutumia kategoria maalumu ya taarifa, taarifa  binafsi za kila aina zitalindwa vya kutosha, kiusahihi na kuhuishwa, huku ikikidhi haki za washiriki. 



TAARIFA ZA  SIRI ZILIZORUHUSIWA KUTOLEWA

Tunaweza kutoa taarifa zako binafsi ikiwa inahitajika kufanya hivyo kulingana na  sheria, au ikiwa tunaamini kwa imani thabiti kwamba kufanya hivyo   ni muhimu: (1) kuzingatia mchakato wowote wa kisheria tunaoutoa, kwenye tovuti zetu zozote au huduma au katika hali fulani ambapo tupo chini ya  wajibu sawa wa kisheria; (2) kulinda na kutetea haki zetu au mali; au (3) kuchukua hatua ili kulinda usalama binafsi wa watumiaji wa huduma au umma. Ikiwa, kwa uamuzi wetu pekee, utaonekana kuwa umedanganya au umejaribu kutulaghai, sisi, kampuni, au mtumiaji mwingine yeyote wa huduma kwa njia yoyote ikiwa ni pamoja na, pasipo ukomo kwa udanganyifu wa mchezo au ulaghai wa malipo, au ikiwa tunakushuku kuwa umefanya malipo ya ulaghai, ikiwa ni pamoja na matumizi ya kadi za benki zilizoibwa, au shughuli nyingine yoyote ya ulaghai (ikiwa ni pamoja na urejeshaji wa malipo ubadilishaji mwingine wa malipo) au shughuli iliyopigwa marufuku (ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha), tuna haki ya kutumia taarifa hizi (pamoja na utambulisho wako) na tovuti nyingine za michezo ya kubahatisha mtandaoni, benki,kampuni za kadi za mkopo, mashirika yanayofaa, na mamlaka zinazohusika. (4) Kwa madhumuni ya utafiti kuhusu kuzuia hitilafu,taarifa inaweza   kutolewa bila majina na kutumwa  katika taasisi inayohusika.

UTUMIAJI

Unaweza ‘kujiondoa‘ kupokea mawasiliano yoyote ya matangazo ama kwa kuchagua kujiondoa kupitiautaratibu uliowekwa  kwa njia  ya akaunti yako inayopatikana kwenye tovuti zetu au huduma au katika baruapepe unayopokea kutoka kwetu, au wakati wowote kwa kutuma baruapepe, au kwa kutuandikia kwenye Huduma kwa Wateja.

Zaidi ya hayo, unaweza kuwasiliana nasi ikiwa: 1) unataka kuthibitisha usahihi wa taarifa binafsi tuliyokusanya kuhusu wewe; 2) ungependa kuhuisha taarifa zako binafsi; na/au 3) una malalamiko yoyote kuhusu matumizi yetu ya taarifa zako binafsi. Ikiombwa, (1) tutahuisha taarifa zozote ambazo umetupatia, iwapo utathibitisha umuhimu wa mabadiliko hayo au (2) kuweka alama taarifa zozote za kuzuia matumizi ya baadaye kwa madhumuni ya uuzaji wa bidhaa zetu. Kwa kutoa shaka, hakuna chochote katika Sera hii ya Siri kitakachotuzuia kuhifadhi maelezo yako ya binafsi ambapo tunatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

TAARIFA SHAMIRISHI

Taarifa zilizomo   kwenye kifaa chako

Wakati wa kutumia huduma zetu, tunaweza kuhifadhi taarifa kwenye kifaa chako. Taarifa  hizi zinajulikana kama taarifa shamirishi , ambayo ni mafaili madogo ya nyaraka ambazo zimehifadhiwa kwenye kifaa chako wakati unapotembelea kurasa za mtandaoni ambazo zinaweka kumbukumbu ya  mapendekezo yako. Pia, tunatumia ‘taarifa shamirishi za kumbukumbu ‘. ‘taarifa shamirishi za kumbukumbu ni sawa na taarifa shamirishi kwenye  kisakuzi. Zinaturuhusu kukumbuka mambo kuhusu mara ngapi umeingia kwenye tovuti yetu. Si taarifa shamirishi wala   kumbukumbu zinaweza kutumika kupata au kutumia maelezo mengine kwenye kompyuta yako. Tunatumia tu njia hizi kufuatilia matumizi yako ya huduma zetu. Taarifa shamirishi hutusaidia kufuatilia msongamano kwenye tovuti, kuboresha huduma zetu na kuifanya iwe rahisi na/au muhimu zaidi kwa matumizi yako. Tunatumia taarifa shamirishi za kumbukumbu na taarifa shamirishi za upande wa tatu ili kutusaidia kukuonyesha matangazo yanayofaa na yanayohitajika zaidi.

Taarifa shamirishi ambazo ni muhimu zaidi

Taarifa shamirishi ni muhimu ili kuruhusu mtumiaji kutembelea tovuti na kutumia vipengele vyake, kama vile kutumia maeneo salama ya tovuti au kufanya miamala ya kifedha. Bila taarifa hizi, tovuti yetu haiwezi kufanya kazi kwa ufanisi.

Wakati wa mchakato wa usajili

Taarifa shamirishi hizi zitabeba taarifa ziliyokusanywa wakati wa usajili wako na zitatusaidia kukutambua kama mteja na kukupa huduma unayohitaji. Tunaweza pia kutumia data hii kuelewa vizuri maslahi yako unapokuwa mtandaoni na kuboresha ziara zako kwenye majukwaa yetu.

Kwenye tovuti yetu

Kwa wageni wanaotembelea kwenye tovuti yetu, tunatumia Taarifa shamirishi kukusanya taarifa. Seva zetu hutumia aina tatu tofauti za Taarifa shamirishi:

Taarifa shamirishi za ‘kipindi maalumu’: Aina hii ya taarifa shamirishi huwekwa tu kwenye kompyuta yako kwa muda unapotembelea tovuti yetu. Taarifa shamirishi  ya kipindi maalumu’hukusaidia kutembelea tovuti yetu kwa kasi na, ikiwa wewe ni mteja uliyesajiliwa, inatuwezesha kukupa taarifa ambazo sahihi zaidi kwako. Taarifa shamirishihizi huisha muda wake kiotomatiki unapofunga kisakuzi chako.

Taarifa shamirishi  ‘endelevu’: Aina hii ya taarifa shamirishi itabaki kwenye kompyuta yako kwa muda uliowekwa kwa kila taarifa shamirishi. Taarifa shamirishi za kumbukumbu pia ni endelevu.

Taarifa shamirishiza ‘Uchambuzi’: Aina hii ya taarifa shamirishi  huturuhusu kutambua na kuhesabu idadi ya wageni wanaofungua tovuti yetu na jinsi wanavyotumia huduma zetu. Msaada huu unaboresha jinsi tovuti zetu zinavyofanya kazi, kwa mfano, kwa kuhakikisha unaweza kupata kile unachotafuta kwa urahisi.

Unaweza kukubali au kukataa taarifa shamirishi. Visakuzi vingi vya wavuti hukubali taarifa shamirishi kiotomatiki, lakini, ikiwa unapenda, kwa kawaida unaweza kurekebisha mpangilio wa kisakuzi chako ili kukataa taarifa shamirishi. Kibainishi cha maudhui katika orodha ya visakuzi vingi itakuelekeza jinsi ya kuzuia kisakuzi chako, kukubali taarifa shamirishi mpya, jinsi ya kuwa na kisakuzi kinachokujulisha unapopokea taarifa shamirishi mpya, na jinsi ya kuzima taarifa shamirishi   kabisa.

Vidokezo vya Taarifa Shamirishi 

Unaweza kurekebisha mipangilio yako ya Programu Tumizi ili kuzuia matumizi ya vidokezo vya taarifa shamirishi. Kisaidizi cha Mpangilio waa programu tumizi hukuruhusu kudhibiti mapendeleo yako. Ili kuzuia vidokezi vya taarifa shamirishi kutoka katika maudhui yote ya upande wa tatu, nenda kwenye kidhibiti uhifadhi wa taarifa ya Kisaidizi cha Mipangilio na kuondoa kisanduku cha kuangalia kilichoandikwa 'Ruhusu programu tumizi ya kutengenezea midia na proramu ya upande wa tatu ili kuhifadhi taarifa kwenye kompyuta yako’ na ufunge Kisaidizi cha Mipangilio. Vinginevyo, unaweza pia kurekebisha mipangilio yako kwa ajili ya tovuti maalumu unazofungua kupitia ‘kidhibiti cha mpangilio wa uhifadhi taarifa cha Tovuti’ ambayo pia hupatikana katika Kisaidizi cha Mipangilio.

Ikiwa unatumia toleo la zamani la Programu Tumizi au kisakuzi cha wavuti cha zamani, Kisaidizi cha Mipangilio huenda kisipatikane kwako. Tunapendekeza kwamba uhakikishe unahuisha Programu Tumizi na kisakuzi chako kwenye matoleo ya hivi karibuni yanayopatikana.

Ikiwa unachagua kukataa taarifa shamirishi, huenda usiweze kupata vipengele vyote vya maingiliano kwenye tovuti yetu.

IDHINI YA MATUMIZI YA WATOA HUDUMA ZA KIELEKTRONIKI

Ili kucheza michezo halisi ya pesa kwenye huduma zetu, utahitajika kutuma na kupokea pesa kutoka kwetu. Tunaweza kutumia mifumo ya malipo ya kielektroni ya upande wa tatu ili kufanya michakato ya miamala hiyo ya kifedha. Kwa kukubali Sera hii ya Siri , unakubali taarifa binafsi muhimu kwa kwa kufanya michakato ya  miamala ikiwa ni pamoja na, inapobidi kufanya, uhamisho wa taarifa zako nje ya nchi yako. Tunachukua hatua  hii ili kuhakikisha kwamba mipango yetu na mifumo ya malipo inalinda siri  zako.

IDHINI YA UKAGUZI WA USALAMA

Tuna haki ya kufanya ukaguzi wa usalama wakati wowote ili kuthibitisha data ya usajili uliyoitoa na kuthibitisha matumizi yako ya huduma na miamala yako ya kifedha ikiwa kuna viashirio vya ukiukaji wa kanuni na Masharti yetu na sheria inayohusika. Kwa kutumia huduma zetu na hivyo unakubaliana na Kanuni na Masharti yetu kwamba unatuidhinisha kutumia taarifa zako binafsi na kuweka wazi taarifa zako binafsi kwa upande wa tatu ili kuthibitisha taarifa unazotoa wakati wa matumizi yako ya huduma zetu, ikiwa ni pamoja na, inapobidi, uhamisho wa taarifa nje ya nchi yako. Tathmini ya usalama inaweza kujumuisha lakini bila ukomo kuagiza ripoti ya mkopo na/au vinginevyo kuthibitisha maelezo unayotoa dhidi ya kanzidata ya upande wa tatu. Zaidi ya hayo, ili kuwezesha tathmini hizi za usalama, unakubali kutoa taarifa au hati hizo pale   tu tutakapokuomba.

USALAMA

Tunaelewa umuhimu wa usalama na mbinu zinazohitajika ili kulinda taarifa. Tunahifadhi taarifa zote binafsi tunazopokea moja kwa moja kutoka kwako katika kanzidata iliyosimbwa na iliyolindwa na nywila iliyopo ndani ya mtandao wetu ulio salama nyuma ya programu tendaji ya ukuta wa moto (firewall) iliyowekwa kwa ufundi  ambayo inasaidia Toleo la 3 SSL pamoja na msimbo wa 128-bit. Pia, tunachukua hatua kuhakikisha matawi yetu, mawakala, washirika, na wauzaji wanachukua hatua za usalama za kutosha.

USALAMA WA WATOTO

Huduma zetu haziruhusu kwa watu walio chini ya umri wa miaka 18 (au umri halali katika mamlaka zao). Mtu yeyote anayetoa taarifa zake kwetu kupitia Huduma zetu zozote anatuhakikishia kwamba ana umri wa miaka 18 (au umri halali katika mamlaka inayohusika) au zaidi. Ni kuhusu  sera yetu kufichua majaribio ya watoto kupata huduma zetu ambazo zinaweza kutulazimu kufanya  a tathmini ya usalama. Ikiwa tunagundua  kuwa mtoto amejaribu au amewasilisha taarifa binafsi kupitia huduma zetu, hatutazikubali taarifa zake na tutachukua hatua za kufuta taarifa hizo kutoka kwenye rekodi zetu.

UHAMISHO WA KIMATAIFA

Taarifa binafsi zilizokusanywa kwenye huduma zinaweza kuhifadhiwa na kuchakatwa katika nchi yoyote ambayo sisi au washirika wetu, wasambazaji, au mawakala huhifadhi vifaa. Kwa kutumia huduma zetu, unakubali uhamisho wowote wa taarifa nje ya nchi yako (ikiwa ni pamoja na nchi ambazo haziwezi kutathminiwa kuwa na sheria za faragha zinazotosheleza). Hata hivyo, tunachukua hatua kuhakikisha kwamba mawakala wetu, washirika, na wauzaji wanazingatia viwango vyetu vya faragha bila kujali eneo lao.

UTENDAJI WA UPANDE WA TATU

Hatuwezi kuhakikisha usalama wa taarifa zozote ambazo upande wa Tatu unatoa kwa tovuti  inayounganisha na au kutoka katika huduma au taarifa yoyote iliyokusanywa na mtoa huduma yeyote wa upande wa tatu anayeongoza programu yetu ya pamoja  (ikiwa inafaa) au programu nyingine yoyote, kwa kuwa tovuti hizi za mtandaoni za upande wa tatu, zinamilikiwa na zinaendeshwa kwa kujitegemea kutoka kwetu. Taarifa yoyote iliyokusanywa na pande hizi inasimamiwa na sera ya siri  ya pande hizo ikiwa ipo.


KANUSHO LA KISHERIA:

Huduma zinafanya kazi ‘KAMA ZILIVYO’ na ‘kama zinavyopatikana’ bila dhima ya aina yoyote. Sisi hatuwajibiki kwa matukio yoyote nje ya udhibiti wetu wa moja kwa moja. Kutokana na hali ngumu na inayobadilika kila mara ya teknolojia na biashara yetu, hatuwezi kukuhakikishia wala kudai kwamba hakutakuwa na hitilafu ya kiutendaji kuhusu siri ya taarifa zako binafsi, na hatutawajibika kwa uharibifu wowote usio wa moja kwa moja, wa bahati mbaya, matukio, au wa adhabu unaohusiana na matumizi au kutolewa kwa taarifa binafsi.

RIDHAA YA SERA   YA SIRI

Matumizi yako ya huduma zetu huunda makubaliano ya Sera yetu ya Siri.

Hii ni sera yetu nzima na ya kipekee ya siri na inachukua nafasi yoyote ya toleo la awali. Sera hii ya siri inapaswa kusomwa pamoja na Kanuni na Masharti yetu na masharti yoyote ya ziada yanayotumika, yaliyopo kwenye tovuti zetu. Tunaweza kufanya mabadiliko ya Sera hii ya siri mara kwa mara na kukujulisha mabadiliko haya kwa kuchapisha kanuni zilizobadilishwa kwenye majukwaa yetu. Kuendelea kwako kutumia huduma zetu kufuatia mabadiliko yoyote ya Sera hii ya Siri ni kwamba unaafikiana na mabadiliko hayo. Tunakushauri uangalie Sera hii ya Siri mara kwa mara.




TOVUTI NYINGINE

Tovuti yetu inaweza kuwa na viungo kwenye tovuti nyingine, ambazo ziko nje ya udhibiti wetu na hazijafanyiwa kazi na Sera hii ya Siri. Ikiwa unatumia tovuti zingine kwa kutumia viungo (link) uliyopewa, waendeshaji wa tovuti hizi wanaweza kukusanya taarifa kutoka kwako, ambazo watazitumia kulingana na sera yao ya siriambayo inaweza kutofautiana na yetu. Kwa hivyo, waendeshaji wa tovuti hizi, watawajibika kutokana na utendaji wao au hitilafu zinazoweza kujitokeza kwenye tovuti zilizounganishwa.

Unapocheza michezo ya kasino iliyotengenezwa na Net Ent, sera ya siri ya Net Ent pia hutumika. Hii inaweza kupatikana kupitia, HYPERLINK "https://www.netent.com/en/netent-privacy-policy-eu/"https://www.netent.com/en/netent-privacy-policy-eu/. 

Washirika wa Thamani
PalmBeachCasinoLasVegasCasinoLeGrandeCasino
Jumla
AviatorMsaadaPromosheni
SHERIA & UTEKELEZAJI
Vigezo na Masharti KiujumlaSera za FaraghaUwajibikaji KimchezoBodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania
Pakua ProgramuIosMarketAndroidMarket
Wasiliana Nasi
1456
Dunia Investment Limited located at 10th Floor Harbour View Towers, Samora Avenue, Dar es Salaam Tanzania is licensed & regulated by the Gaming Board of Tanzania under licenses SBI000000021, SBPO00000016 and OLC000000003.
FastHubFastHubHalotelFastHubTigoAirtelVodaselcom
logo
© 2026 Pigabet | Haki Zote Zimehifadhiwa.
Cheza Kistaarabu18+
logo