IMETOLEWA NA BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA TANZANIA
Sera ya Michezo ya Kubahatisha
Pigabet imedhamiria kuidhinisha mchezo wa kubahatisha wa kistaarabu miongoni mwa wateja wake pamoja na kuongeza ufahamu wa matatizo yanayotokana na michezo ya kamari na kuboresha uzuiaji, kuingilia kati, na suluhisho .
Sera ya uchezeshaji wa kistaarabu wa Kamari ya Pigabet inadhamiria kupunguza madhara yanayotokana na uchezaji wa kamari na kuhamasisha uchezaji ulio wa kistaarabu.
Pigabet husaidia kizazi cha wacheza kamari mtandaoni kuwapa aina ya michezo na burudani mbalimbali. Pia, tunachukua jukumu la kupanga bidhaa zetu.
Pigabet inalenga kuanda jukwaa la michezo ya kubahatisha lenye salama zaidi na ubunifu zaidi kwa watu wazima. Bidhaa zinazopatikana bila kikwazo na salama zinazotolewa huruhusu kila mtumiaji kucheza kulingana na uwezo wake wa kifedha na kupokea huduma bora zaidi. Uadilifu, haki, na uaminifu ni kanuni zinazoongoza za kazi ya Pigabet. Kwa hiyo ni wazi kwamba Pigabet inapaswa kujitahidi kuepuka na kupunguza matatizo ambayo yanaweza kutokea kutokana na kushiriki katika kamari, hasa katika sual la uchezaji usio na kiasi. Wakati huohuo, ni muhimu kuheshimu haki za wale wanaoshiriki katika michezo ya kubahatisha kwa kadiri iwezekanavyo kama njia ya burudani.
Uchezaji wa kistaarabu wa Kubahatisha katika Pigabet unategemea kanuni tatu za msingi: Usalama wa mchezaji, Usalama wa mchezo, na Ulinzi dhidi ya uraibu wa kamari. Pamoja na taasisi za utafiti, vyama, na taasisi za tiba, tunafanyakazi kwa ustaarabu, usalama, na mpango kazi wa kuaminika wa michezo ya kubahatisha mtandaoni.
Usalama wa mchezaji
Tunawajibika kwa usalama wa wachezaji wetu. Usalama wa wachezaji unajikita kukataza ushiriki wa watoto (watu chini ya umri wa miaka kumi na nane (18)) kushiriki katika michezo na ulinzi wa faragha, ambao unahusisha uchakataji wa kistaarabu wa taarifa binafsi na malipo. Haki na usawa wa huduma zinazotolewa zina fuatiliwa kwa karibu na mashirika yanayojitegemea. Mawasiliano ya masoko pia yanalenga usalama wa mchezaji na tunaahidi kuwa wachezaji tu ndio wanaweza kupokea huduma zetu kwa uwazi.
Ulinzi dhidi ya uraibu wa michezo ya kubahatisha: utafiti – kuzuia – kuingilia kati
Wachezaji wanaocheza mchezo wa kubahatisha wa mpira wa miguu, mchezo wa kasino, na michezo mingine ya kubahatisha, zaidi hucheza kwa ajili ya burudani. Mazoea na mifumo fulani ya tabia (kama vile ununuzi, kucheza michezo, kula, au matumizi ya pombe) ambayo inachukuliwa kuwa ya kawaida na isiyosababisha wasiwasi wowote inaweza kukuza mazoea kwa watu wengine na kusababisha matatizo. Kwa namna hiyohiyo, michezo ya kamari inaweza kusababisha matatizo kwa kundi dogo la wateja.
Wateja walioathirika na michezo ya kubahatisha wamepigwa marufuku kuendelea kushiriki katika safu ya michezo ya kubahatisha. Wakati mwingine , wateja hawa hupewa mawasiliano ya mashirika ambapo wanaweza kupata ushauri wa kitaalamu na msaada.
Ushiriki binafsi ni njia endelevu zaidi ya kujizuia
Kanuni ya msingi inayokuzwa na Pigabet ni kwamba uamuzi wa mwisho na wajibu kuhusu kucheza au kutocheza, na kiasi gani cha fedha kinaweza kutumika kwenye mchezo lazima kiamuliwe na mteja mwenyewe. Uwajibikaji binafsi wa mteja kwa hiyo ni njia bora zaidi ya ulinzi dhidi ya uraibu. Pigabet inaona kuwa ni wajibu wake katika kusaidia wateja wake kwa kutoa huduma kwa uwazi, na taarifa kamili, na kuweka mpangilio wazi wa mwenendo utendaji.
ULINZI WA WATOTO
Pigabet hairuhusu watoto (chini ya umri wa miaka 18) kushiriki katika michezo na kubashiri. Ndiyo maana uthibitisho wa kuwa umefikia umri wa mtu mzima na uthibitisho wa tarehe ya kuzaliwa ni mahitaji ya lazima wakati wa kufanya usajili. Pigabet inazingatia suala la watoto kushiriki katika michezo na kamari kwa umakini sana. Ili kuwapa ulinzi ulinzi bora zaidi watoto, tunategemea pia msaada wa wazazi na walezi. Tafadhali weka taarifa zako ili utumie akaunti kwa usalama (Jina na nenosiri).
Zaidi ya hayo, tungependekeza kwamba uweke maunzi laini ya kuchuja taarifa. Maunzi laini hii itakuwezesha kuzuia upatikanaji wa huduma za mtandao zisizofaa kwa watoto na vijana.
Wajibu wa kukabiliana na matatizo
Pigabet inaedesha aina nyingi za michezo ya kubahatisha ambayo ni mifumo ya burudani kwa wateja wengi. Wakati huohuo, kampuni inachukua jukumu kwa wateja wake kwa kutoa msaada na zana kwa ajili ya matengenezo ya mazingira salama na ya burudani kwa kuzingatia vihatarishi vinavyohusiana.
Wateja ambao wanapata shida katika kutathmini hatari, na kutambua mipaka yao wenyewe, au wale ambao wanakabiliwa na uraibu wa kamari hawawezi kufurahia utaratibu wa wa huduma zetu ipasavyo na kuona kama hii ni aina ya burudani. Pigabet inawajibika kwa watumiaji kama hao kuzuia kupata huduma zake kwa ajili ya ulinzi wao wenyewe.
Kupata taarifa kuhusu masuala ya msingi!
Watu wengi hucheza kwa ajili ya burudani. Ushiriki wa kawaida katika katika michezo kulingana na uwezo wao wa kifedha unakubalika. Hata hivyo, kwa asilimia ndogo ya watu wanaocheza kamari ambapo kwao si aina ya burudani, ni changamoto ambayo lazima ikabiliwe kwa umakini.
Tabia inayochochea matatizo ya michezo ya kubahatisha ni nini?
Tabia inayochochea matatizo ya michezo ya kubahatisha inachukuliwa kuwa tabia ambayo inaingilia hali ya maisha, kazi, nafasi ya kifedha, au afya ya mtu au familia yake. Kushiriki kwa muda mrefu katika michezo ni ishara mbaya kwa mtu kama huyo kwani kunaweza kusababisha matokeo mabaya.
Mnamo 1980 utegemezi wa patholojia ya mchezo wa kubahatisha umetambuliwa rasmi na kuorodheshwa katika orodha ya magonjwa ya kisaikolojia katika Mfumo wa Kimataifa wa Uainishaji wa DSM-IV na ICD-10. Huu huchukuliwa kama ni kipindi kirefu, kurudiwa, na mwelekeo wa kukuza michezo hiyo, licha ya kuwa na hali mbaya ya binafsi na hata kijamii, kama vile madeni, kuvunjika kwa uhusiano wa kifamilia, na kudumaa kwa ukuaji wa kitaaluma.
Ni kwa kiwango gani tabia ya mtu inaweza kuchukuliwa kama ni utegemezi?
Ni muhimu kusisitiza kwamba, uchunguzi wa ugonjwa wa utegemezi wa mchezo unaweza kuelezewa na wataalam tu. Nyenzo zilizowasilishwa kwenye ukurasa wa wavuti wa Pigabet (www.pigabet.co.tz) zitakusaidia kukadiria na kufafanua tabia yako ya mchezo.
Hatari ya uraibu ambayo haihusiani na kitu chochote ni kwamba ni vigumu sana kuelezea utofauti kati ya burudani na uraibu. Hata hivyo, baadhi ya ishara za uchunguzi zinaweza kuonyesha matatizo yaliyopo. Kuwa na angalau dalili tano kati ya hizi zifuatazo, uwezekano wa utegemezi mkali au mkubwa, huwa na dalili zifuatazo:
Mchezaji hujihusisha sana na kamari, mawazo yake yote yanahusu mchezo huo tu.
Kutumia muda mrefu kupindukia katika kucheza mchezo wa kubahatisha.
Majaribio ya kuacha au kudhibiti ushiriki wake katika michezo yanaonekana kuwa hayafanikiwi.
Anapopunguza ushiriki wake katika kamari, hupata hamu ya kuendelea na kukata tamaa ya kuacha.
Mchezo ndiyo njia ya kuepuka matatizo au usumbufu.
Mchezaji hujaribu kurudisha kiasi kilichopotea,
Huongopa kuhusu tabia yake ya kucheza,
Hufanya vitendo haramu,
Huharibu au kuvunja uhusiano na familia na wenzake,
Hukopa ili kushiriki katika michezo ya kamari.
Kanuni za kujihusisha na michezo ya kubahatisha
Kufuatia kanuni zilizowekwa hapa chini, unaweza kufurahia mchezo ya kubahatisha bila wasiwasi:
Anza kucheza pale tu unapokuwa na amani na kuzingatia.
Fanya mapumziko ya mara kwa mara.
Jitathmini mwenyewe kabla kiasi cha mwezi utakachoweza kutumia kwa ajili ya mchezo ya kubahatisha.
Utakapojiwekea kiwango cha juu, usiiongeze zaidi.
Kabla ya kuanza kucheza, tathmini makadirio ya juu ya kushinda, baada ya kufikia makadirio hayo unapaswa kuacha kucheza.
Tathmini mapema kiasi ambacho unaweza kupoteza.
Usianze kucheza ukiwa umelewa
Usianze kucheza ukiwa katika hali ya mawazo.